Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe amefunguka na kutoa ya moyoni kwa mara ya kwanza tangu aondolewe katika kiti cha urais kufuatia mapinduzi ya kijeshi.

Robert Mugabe amesema hajawahi kufikiria kwamba Rais mpya Emmerson Mnangagwa atamgeukia na amelaani kitendo cha kuondolewa madarakani.

“Sikufikiria kabisa kwamba mtu ambaye nimemjenga na kumleta katika serikali na juhudi kubwa niliofanya kuokoa maisha yake alipokuwa jela alipokuwa ametishiwa kunyongwa, kwamba siku moja atakuwa ndiye mtu atanigeukia,” Mugabe.

Amezungumza hayo katika mahojiano na shirika la utangazaji la Serikali la Afrika Kusini SABC akiwa Harare.

Mugabe mwenye umri wa miaka 94, ameiongoza Zimbabwe tangu kupata uhuru mwaka 1980 mpaka aliposhinikizwa kuachia madaraka na washirika wa Mnangagwa walioko katika jeshi la nchi hiyo Novemba mwaka 2017.

Mugabe ni moja ya watu shujaa nchini humo kutokana na harakati za ukombozi alizoziendesha nchini kwake.

Kwa upande mwingine Mugabe analaumiwa kwa kusababisha uchumi wa Zimbabwe uliokuwa imara kuharibika na nchi hiyo kutengwa kimataifa.

Aidha Mnangagwa, aliyekuwa makamu wa rais chini ya Mugabe, ameahidi kukaribisha wageni kuja kuwekeza nchini humo na pia kurejesha mahusiano na nchi za Magharibi baada ya kuchukua madaraka.

Mnangagwa alihukumiwa kunyongwa kwa kosa la uhujumu chini ya utawala wa wazungu waliowachache. Lakini alisamehewa kunyongwa kwa sababu ilionekana kuwa alifanya kosa hilo wakati akiwa mtoto mdogo.

 

Video: DataVision, MacLeans BeneCIBO zarudisha tabasam la mtoto Mariam
Makonda awapa kibali wasanii kurekodi kazi eneo lolote