Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson leo (Aprili 03, 2018) amewaapisha wabunge wawili wapya, ambao ni Dkt. Godwin Mollel wa Jimbo la Siha pamoja na Maulid Mtulia kutokea Jimbo la Kinondoni.

Wabunge hao wameapishwa baada ya kufanyika uchaguzi mdogo wa marudio katika majimbo hayo mawili ambayo hapo awali yalikuwa hayana wawakilishi bungeni kutokana na viongozi wake kujiuzulu nyadhifa zao kwa kuhamia chama kingine na kukiacha kile cha awali walichopigiwa kura na wananchi wao.

Aidha, kiapo hicho cha leo kimeshuhudiwa na idadi ndogo ya wabunge wa upinzani kutokana na baadhi yao kuwepo Mahakamani kusikiliza mwenendo wa kesi yao inayotarajiwa kuung’uruma leo katika viwanja vya Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.

Kutokana na kiapo hicho, Mtulia na Dkt. Mollel watakuwa wamekubali moja kwa moja kubeba mizigo ya matatizo kutoka kwa wananchi wao ambayo ilikuwa ikiwasumbua kipindi kirefu pamoja na kuwatekelezea ahadi walizokuwa wamezitoa kipindi walichokuwa wanaomba ridhaa ya kupigiwa kura ya ndio ili waweze kuwa Wabunge katika majimbo hayo.

Masogange ahukumiwa kifungo jela
Video: Usione Simba kalala ukamchezea sharubu- JPM, Maandamano kutikisa ukuta Mererani