Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, limemfikisha Mahakamani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mousa Twaleb (46), ambaye anatajwa kuwa ni dereva teksi akituhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuhusika kumteka mfanyabiashara Mohammed Dewji.

Tukio la kutekwa kwa Mohammed Dewji lilitokea Oktoba 11, 2018 ambapo kupitia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam alieleza jeshi hilo lilikuwa likiwashikilia baadhi ya watu wakituhumiwa na tukio hilo.

Mohammed Dewji alitekwa akiwa jijini Dar es salaam alipokuwa akitokea kwenye mazoezi katika Hoteli ya Colloseum ambapo washukiwa wa awali waliotajwa na polisi walikuwa ni raia wa kigeni.

Aidha, machi 4, akiwa Ikulu jijini Dar es salaam wakati wa zoezi la kuwaapisha Makamishna wa juu wa jeshi la polisi pamoja na mawaziri wapya wawili akiwemo Waziri wa Katiba na Sheria na Dkt Agustine Mahiga pamoja na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi, Rais Magufuli alihoji kuhusu suala hilo.

“Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo Dewji linaacha maswali, tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa, tulionyeshwa nyumba na dereva lakini hadi leo hakuna aliyepelekwa Mahakamani hata kama,” alisema JPM

Mo Dewji alipatikana Oktoba 20, 2018.

Watuhumiwa wa 'Tereza' watiwa mbaroni
Uganda: Wanaosaidia ombaomba kufungwa