Mtoto wa miezi mitano Jijini Dar es salaam, katika hospitali ya Muhimbili amekatwa kiganja cha mkono wake wa kushoto baada ya kupatiwa huduma za matibabu ya sindano kupitia mshipa wa mkononi na kupelekea mkono huo kuharibika na kukatwa kabisa.

Matibabu hayo alikuwa akifanyiwa katika hospitali ya Mwananyamala ambapo baadae alipewa rufaa katika hospitali ya Muhimbili baada ya kuona hali ya mtoto inazidi kuwa mbaya na mkono ukizidi kubadilika rangi na kuwa mweusi huku ukisinyaa.

Mama wa mtoto huyo alianza kuona mkono wa mtoto wake ukibadilika lakini mara baada ya kuripoti hali hiyo kwa madaktari hospitali ya Mwananyamala walisema kuwa damu imevilia hivyo walimshauri mama huyu kuchukua mkono wa mwanae na kuweka kwapani hadi utaporudi katika hali ya kawaida.

Mama huyo alieleza hayo pindi alipohojiwa na chombo cha habari cha TBC, na kusema kuwa chanzo kilichopelekea mtoto wake kufikia hatua hiyo ni kutokana na kanyula aliyowekewa siku chache zilizopita alipofika kufanyiwa matibabu baada ya kushikwa na homa kali.

”Tatizo ni kanyula vidole viwili vikawa vyeusi, alivyofungua kiganja chote hiki kikawa cheusi vidole vitatu vikabaki, baada ya hapo nikaambiwa damu itakuwa imevilia nikaambiwa niviweke kwapani, nikamuweka kwapani, hivyo mtoto akawa anachoma sindano za matakoni, hawakumwekea tena kanyula, baada ya hapo, jumamosi jioni dokta wa watoto akapita, nikamuonyesha, dokta akasema muweke kwenye kwapa damu imevilia kadri siku zionavyoenda mkono unazidi kubadilika, jumamosi jioni mkono ukasinyaa, nikarudi tena kwa daktari..”

Akiendelea kuhadithia mama huyo anasema Jumapili, siku iliyofuata aliambiwa ampeleke mtoto kwa madaktari wa upasuaji ndipo alipopewa rufaa ya kwenda kufanyiwa matibabu zaidi katika hospitali ya muhimbili.

Alipofika katika hospitali ya Muhimbili baada ya daktari kumuangalia mtoto tayari alikuwa amesha gundua tatizo hivyo aliamuru mtoto yule apelekwe chumba cha upasuaji kwa ajili ya kukatwa mkono kwani tayari sumu ile ilikuwa imeanza kusambaa mwilini.

Hata hivyo mama wa mtoto aliomba kabla ya mtoto wake kukatwa mkono aliomba vipimo viafanyike ili aweze kugundua tatizo hasa lilikuwa nini, siku ya jumatano aliamkia vipimo na kugundua kuwa baada ya kuwekewa kanyula kwenye mshipa akawekewa kwenye maungio ya kiganja.

Tekla Gabriel ambaye ni dada wa mama Yvone ameomba serikali kupitia Wizara ya Afya kulitazama kwa kina suala hilo na kulisimamia kuhakikisha hospitali iliyohusika na kumsababishia binti yao ulemavu wa maisha wanawajibishwa kulingana ana sheria ya nchi kwani wao wanaona kilichifanyika ni uzembe wa madaktari.

Mganga mkuu wa Hospitali ya Mwenanyamala Daniel Mkungu,  ameiambia TBC kuwa kitaalamu haiwezekeni kanyula kusababisha mishipa ya damu kuziba kwani kwenye kiganja kuna mishipa mingi ya damu hata mshipa mmoja ukiziba mishipa mingine huendelea kufanya kazi kama kawaoda.

Ameongezea kuwa hakuna uzembe wowote uliotokea kwani mtoto yule alikuwa anaangaliwa kila siku na katika wodi ya watoto yupo mtaalamu wa watoto ambaye muda wote anakuwa humo.

Pia TBC ilifanikiwa kugonga hodi katika kwa Afisa Uhusiano Hospitali ya Muhimbili, Aminieli Aligaisha ambapondipo alipofanyiwa upasuaji wa kiganja chake anasema mama alielezwa kilichosababisha mtoto wake kukatwa mkono.

Amesisitiza malalamiko ya mama Yvona ni ya msingi kabisa, na ameomba mtu wa tatu aweze kuingilia kati ili kutolea uamuzi suala hilo.

Hata hivyo mwanasheria, Seif Ngalinda aliyetafutwa na kuhojiwa juu ya jambo kama hilo na kusema kuwa

”Katika sheria zetu kuna sheria ya madhara sheria hii inatoa adhabu endapo mtu mwenye jukumu fulani ama taaluma anapofanya jambo kinyume na taaluma yake kama ambavyo inatakiwa kufanywa, hivyo kwa daktari anatakiwa atoe huduma kwa mgonjwa kwa kiwango cha hali ya juu, hivyo katika sheria ya madhara ikathibitika kuwa kuna uzembe atatakiwa kulipa fidia na ndugu hawa wanaweza kufungua shitaka la madai kwa hospitali na mshauri ambao ndio waajili wa madaktari hao.

 

Makonda atoa ruksa watumishi wa dini kuhubiri klabu na disko usiku
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 9, 2019