Mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya Msingi Jitegemee Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoani Pwani nchini Tanzania amekutwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa katika nyumba ambayo haijakamilika ujenzi.

Manafunzi huyo ambaye inadaiwa alipotea tangu January 14,2020 na taarifa zake kutolewa na ndugu kwa Jeshi la Polisi mkoani Pwani inaelezwa mwili wake umekutwa na michubuko sehemu za siri tukio ambalo linaleta hofu huenda alifanyiwa vitendo vya ubakaji kabla kuuawa.

Kamanda wa polisi mkoani humo Wankyo Nyigese amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akieleza kuwa mwili huo umepatikanaJanuary 19,2020 asubuhi.

Wankyo amesema awali kabla ya tukio hilo mwanafunzi huyo aliondoka nyumbani kwao akiwa na shangazi yake Agnes Peter kwenda gulioni maeneo ya mwendapole kwa shughuli za biashara.

”Ilipofika saa 12 jioni shangazi wa mtoto huyo alimruhusu aende nyumbani kwa maandalizi ya kesho yake , baada ya gulio kuisha Agnes alipofika nyumbani hakumkuta mtoto” amesema

Kamanda Wankyo amesema jitihada za kuwasaka watu waliofanya mauaji hayo zinaendelea na kuwataka wananchi watoe taarifa Polisi au serikali za mitaa.

 

 

Video: Makonda amfunda, Samatta, TFF wataja majukumu yake
Laini za simu kuzimwa kwa awamu