Mtoto wa Kitanzania amerudishwa nchini baada ya wazazi wake kuhukumiwa kunyongwa nchini China kwa kukutwa na madawa ya kulevya.

Baraka Malali na mkewe Ashura Mussa walikamatwa nchini China Jan. 19 mwaka huu kwenye uwanja wa ndege wa Baiyun Guangzhou, wakiwa wamemeza tumboni dawa za kulevya, walihifadhiwa kwenye chumba maalum kwa muda ambapo Baraka alitoa pipi 47 kwa njia ya haja kubwa, huku mkewe akitoa pipi 82.

Aidha, Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa wameongozana na mtoto wao mwenye umri wa miaka 2 na miezi 9. ambapo Serikali ya China iliwasiliana na serikali ya Tanzania kuhusiana na suala la mtoto huyo ndipo walipokubaliana kumrudisha mtoto huyo nchini.

Video: JPM amuapisha Dkt. Slaa kuwa balozi
Dkt. Slaa kuapishwa rasmi leo kuwa balozi Sweden