Uongozi wa timu ya  Mtibwa Sugar umesema kuwa kubadilishwa kwa ratiba ya mchezo wao dhidi ya Simba uliopangwa kuchezwa Septemba 18 na kurudishwa nyuma mpaka Septemba 13 uwanja wa Uhuru sio kikwazo kwao katika harakati zao za kupata ushindi.

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa hakuna kitakachowazuia wao kufanya vyema kwenye mchezo wao wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Simba.

“Timu ikiwa imejiaandaa kutafuta matokeo hakuna kinachoweza kuzuia kupata ushindi, sasa kwa kuwa ratiba imebadilika kwetu sio tatizo tutawafuata Simba kwa tahadhari tukizitafuta pointi tatu hata ingekuwa leo hakuna kinachoshindikana,” amesema Katwila.

Mtibwa inawasili Dar es Salaam kesho kwa ajili ya kuivaa Simba ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wake wa kwanza mbele ya Lipuli kwa kufungwa mabao 3-1 na Lipuli FC.

JPM afanya uteuzi mwingine mkuu wa JKT
Kocha Simba: Tunatoka na ushindi kwa Mtibwa