Matangazo ya biashara sasa kuanza kupata nafasi ya kurushwa kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp kwenye sehemu ya status.

Taarifa hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Mtandao huo, Chriss Daniel.

Japokuwa bado hajatoa ufafanuzi wa kina ni lini biashara hiyo itaanza rasmi na namna gani matangazo hayo yatafanya kazi hali kadhalika na jinsi watu watavyokuwa wananufaika kupitia matangazo hayo.

Whatsapp status inafanya kazi kama ambavyo Insta story kwenye mtandao wa Instagram inavyofanya kazi kwani watu wana uwezo wa kuweka picha, video, kuandika ujumbe wowote vinavyodumu kwa masaa 24.

Mtandao huo wenye watumiaji zaidi ya bilioni 1.5 duniani kote ulinunuliwa na kampuni ya mtandao wa Facebook miaka 4 iliyopita kwa dola bilioni 19 sawa na pesa za Kitanzania trilioni 43 na zaidi

 

Kesi ya Wema yapelekwa mbele, aachiwa huru kwa dhamana ya mamilioni
Usher aiomba mahakama usiri wa gonjwa la ngono

Comments

comments