Mwili wa Steven Weber raia wa Marekani, aliye kufa maji akiwa na mchumba wake Kenesha Antoine, kisiwani Pemba, umekabidhiwa  kwa Ubalozi wa Marekani hapa nchini kwajili ya uchunguzi zaidi.

Weber pamoja na mpenzi wake  walifika visiwani humo kwaajili ya mpaumziko, anadaiwa kufa maji wakati akiogelea kutoka chini ya bahari usawa chumba hicho alikokwenda kumuonyesha mpenzi wake ujumbe wa mapenzi aliomuandikia pamoja na pete kupitia kioo ambacho mtu aliyepo chumbani anaweza kushuhudia kila kitu kinachoendelea chini ya maji.

Wawili hao walitokea eneo la Boton Rounge mjini Luoisian Marekani, walipanga chumba chumba hicho kilichozungukwa na vioo kilichopo chini ya maji katika hotel moja kisiwani Pemba.

Ujumbe ulioandikwa kwenye karatasi hiyo ulisomeka ”siwezi kuzuia pumzi yangu kwa muda mrefu ili kukwambia kila kitu ninachokipenda kwako lakini kila kitu ninachokipenda kwako nakupenda zaidi kila siku”ulisomeka ujumbe huo.

Baadaeye weber alibadirisha karatasi hilo ili kuonyesha maneno aliyokuwa ameandika upande wa pili yaliyosomeka ”Je tafadhali unaweza kuwa mke wangu?utafunga ndoa nami?.

kwa mujibu wa shirika la habari la Marekani CNN, Weber alitoa pete ya uchumba kutoka katika mfuko wake kabla ya kuogelea na kuondoka eneo hilo.

Hata hivyo Antoine alichapisha picha za kisa hicho katika mtandao wa facebook ambapo anaonekana akifurahi pamoja na tamko lake Ndio ndio, lakini mrembo huyo baadaye alichapisha habari mbaya kwamba mpenzi wake amefariki dunia, Antoine alisema hakurudi akiwa mzima baada ya kuogelea baharini.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema mtalii mmoja wa Marekani amefariki nchi Tanzania lakini hakuna maelezo zaidi yaliyo ripotiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari visiwani humo katibu mtendaji Kamisheni utali Zanzibar Abdallah Mohamed, alisema taarifa kutoka kituo cha Konde, Pemba zinaeleza mtalii huyo alifariki akiwa anaogelea, na  mwili wa Weber umechukuliwa na ubalozi wa Marekani kwaajili ya uchunguzi zaidi.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 24, 2019
Ndege ya jeshi yatua Serengeti kubeba mwili wa mtoto wa Jenerali Mabeyo