Katibu Mkuu wa chama cha Wafanyakazi nchini (TUCTA), Yahaya Msigwa amezungumzia kauli ya Rais Magufuli juu ya kutoongeza mshahara kwa wafanyakazi, jambo ambalo limeonekana kuibua hisia hasi kwa watu wengi wakiwemo wanasiasa na wafanyakazi.
 
Msigwa amesema kuwa wao kama wawakilishi wa wafanyakazi, wanakusudia kufanya kikao maalum kujadili suala hilo, na kisha kulijadili na serikali kuangalia njia mbadala na muafaka.
 
“Mambo ya mishahara ni mambo ya utatu yaani wafanyakazi, waajiri na serikali, na mambo haya yanahitaji kujadili kwenye bodi, wafanyakazi wangependa kila mwaka kama inawezekana wawe wanapandishiwa mshahara, kwa hiyo hilo tutalijadili kama wafanyakazi halafu badaye tutajadiliana nao serikali”, amesema Msigwa.
 

Hata hivyo, jana kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei Mosi yaliyofanyika mkoani Iringa Kitaifa, Rais Magufuli amesema hatoongeza mshahara wa wafanyakazi kwa sasa kutokana na serikali kujikita kwenye uboreshaji wa miundombinu.

Kanye West awakera Wamarekani weusi
Manara awatoa hofu mashabiki wa Simba SC, ''nawezaje kuwaacha simba?''