Mshtakiwa Faraji Ramadhani (27) ameiomba mahakama imruhusu ajidhamini mwenyewe kutokana na sehemu zake za siri kutoweka, hivyo kupata maumivu makali anapokuwa mahabusu.

”Hakimu mimi nilikua na mahusiano ya kimapenzi na mtoto wa shekhe, ustadhi huyo alinionya sana kuachana na binti yake lakini sikusikia.

”Hicho ndicho chanzo cha hali hii tatizo la kupotea kwa sehemu zangu za siri, hivyo nikiwa nyumbani huwa natumia dawa nyingi za miti shamba kutuliza maumivu, ”alisema Ramadhani.

Ramadhani, aliwasilisha maombi hayo jana mbele ya hakimu Diana Manase wa Mahakama ya mwanzo jijini Mbeya kesi yake ilipotajwa.

Alimuomba hakimu huyo akubali kujidhamini kutokana na tatizo linalomkabili kwa sababu anapatwa na maumivu makali kila wakati.

Kutokana na malalamiko hayo, Hakimu Manase alimtaka askari aliyekuwepo mahakamani hapo kumkagua mshtakiwa huyo ndipo alipogundua kilichosemwa ni kweli.

Hata hivyo hakimu Diana aligoma kumruhusu ajidhamini kwa madai kuwa endapo atatoroka hawezi kujua sehemu ya kumpata.

Alimtaka aendelee kuvumilia kutokana na tatizo hilo kalitafuta mwenyewe kwa kuwa shekhe huyo alishamuonya aachane na binti yake  akaendelea kukaidi.

Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na shtaka la wizi wa kompyuta mpakato yenye thamani ya sh. 180,000.

Akimsomea shtaka hilo karani wa mahakama hiyo, Tumani Sanga alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo septemba 19 mwaka huu eneo la Mwakibete kwa kuiba kompyuta hiyo mali ya Benson Jaili.

Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa alikana na kurudishwa rumande kutokana na kukosa mdhamini.

Kesi hiyo itatajwa tena Septemba 27, mwaka huu kwaajili ya kusikilizwa.

Vijana washauriwa kuacha dhana ya kuajiriwa
Moto wateketeza Vichanga Wodini