Ligi kuu Soka Tanzania Bara itaendelea leo, Septemba 16 kwa jumla ya mechi 5 kuchezwa  katika viwanja vya miji mbalimbali.

Mabingwa watetezi klabu ya Yanga itakuwa ugenini kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea kuwakabili wenyeji Majimaji. Yanga tayari ina alama 4 kwenye mechi zake mbili za mwanzo ambapo ikishinda mchezo wa leo itakuwa sawa na Azam FC ambayo ina alama 7.

Mechi nyingine ya kusaka uongozi wa ligi hii leo ni kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Mbao FC kwenye uwanja wa Manungu Turiani. Mtibwa Sugar ina alama 6 baada ya kushinda mechi zake mbili za mwanzo hivyo itakuwa inasaka alama zingine 3 ili kufikisha alama 9 na kuongoza ligi kwenye raundi ya 3.

Timu zingine ambazo zina nafasi ya kuongoza msimamo ni Prisons ambayo leo inacheza na Ndanda FC, wakati Lipuli ambayo ina alama 4 itakuwa uwanjani kumenyana na Ruvu Shooting. Endapo Prisons na Lipuli zitashinda wakati huo Mtibwa na Yanga zikapoteza au kutoa sare basi timu hizo zitakwea kileleni kwa kutegemea na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Kesho klabu ya Simba itashuka dimbani kuchuana na Mwadui FC wakati Mbeya City watakuwa wenyeji wa Njombe Mji.

Ben Pol: Tumepenya kikamilifu Nigeria
Video: Balaa laanza kibano makinikia, Maombezi ya Tundu Lissu ngoma nzito

Comments

comments