Mshambuliaji wa Yanga Sadney  Urkhob, kama alitoa ‘gundu’ la kutokufunga kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara baada ya kuwa shujaa wa kikosi hicho  kwa kufunga bao moja pekee la ushindi mbele ya Mbao kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba.

Urkhob ambaye ni raia wa Nambia ametumia jumla ya dakika 360 ambazo ni sawa na michezo minne kuweza kufunga bao katika mchezo huo wa  ligi kuu bara.

Mchezo huo uliopigwa jana ulikuwa na ushindani mkali kwa timu zote mbili ambapo iliwabidi Yanga wasubiri mpaka dakika ya 57 kipindi cha pili kupachika bao la kuongoza na la ushindi ambalo lilidumu mpaka dakika ya tisini.

Ushindi huo unawanyanyua Yanga kutoka nafasi ya 15 ambapo ilikuwa na alama zake 4 mpaka nafasi ya 10 ikiwa na pointi 7 baada ya kucheza michezo 4.

Kufungwa kwa bao hilo kumeifanya Yanga ifikishe mabao manne msimu huu ambapo mawili yamefungwa na David Molinga ‘Falcao’ na moja lingine likifungwa na Mrisho Ngassa.

Mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Pyramids ya Misri ambao ni wa Kombe la Shirikisho utachezwa uwanja wa CCM Kirumba.

Wataalamu wa maendeleo ya jamii watakiwa kutoa takwimu sahihi
Mitihani ya kiswahili kufanyika kimataifa