Msaidizi wa aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa serikali ya awamu ya Nne, Benard Membe, Allan Kiluvya aliyedaiwa kutekwa amepatikana katika maeneo ya Tabata Segerea jijini Dar es salaam.

Akizungumza kwa namna alivyoachwa njia panda ya Segerea amesema kuwa watekaji walimuuliza mahari ambapo ni salama ili waweze kumshusha kutoka ndani ya gari ili asiweze kuzulika.

”Watekaji waliniuliza ni wapi tukikushusha unaweza kufika salama? Nikawauliza kwani tupo wapi? Wakasema tupo Gongo la Mboto. Nikasema mimi nakaa Kinyerezi mkinishusha njia panda ya Segerea nitakuwa salama.”amesema Kiluvya

Amesema kuwa baada ya kumuuliza wamshushe wapi aliwaelekeza sehemu ambayo ni salama ili aweze kushushwa na kuchukua usafiri wa kurudi nyumbani kwake bila ya kupata bughuza yeyote.

Aidha, amesema kuwa kwasababu suala hilo liko Polisi kwasasa hawezi kuelezea ni nini kilitokea huko alikokuwa bali anasubiri tamko au ripoti ya Polisi kwakuwa yeye ni msema kweli.

Lakini pia alipohojiwa kama ataendelea kuwa Msaidizi wa Membe, Allan amesema kuwa anatumaini ataendelea kuwa Msaidizi wa Waziri huyo wa zamani kwani amekuwa msaidizi wake tangu mwaka 2012 akiwa Mwanafunzi wa Chuo hadi sasa

Hata hivyo, ametoa shukrani zake kwa Wanahabari kwa namna ya walivyojitolea kuhakikisha sauti za familia yake, Wanasiasa na Watanzania wote zinasikika. pia amemshukuru Membe, IGP Sirro na Polisi wote wa Kituo cha Kawe.

Tulishamsahau Gadiel Michael, tumesajili wazuri kuliko yeye- Yanga
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 10, 2019