Mwenyekiti wa umoja wa wazazi CCM mkoa wa Arusha, Dk. John Pollangyo, ameshinda kwa kishindo kinyang’anyiro cha kura za maoni ndani ya chama hicho kwaajili ya kupata mgombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki.

Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo hilo lililokuwa likishikiliwa na Joshua Nassari wa Chadema, umepangwa kufanyika Mei 19 mwaka huu, baada ya Mahakama kuu ya kanda ya Dodoma kutupilia mbali kesi ya kupinga kung’olewa.

Katika uchaguzi huo wagombea 33 wakiwemo wanawake watatu walijitokeza kuchukua fomu kwaajili ya kuwania kuteuliwa na chama hicho.

Akitangaza matokeo hayo, msimamizi wa uchaguzi ambaye ni katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa NEC ya CCM, itikadi na uenezi ambaye pia ni mlezi wa chama hicho mkoa wa Arusha, Humphrey Polepole, amesema kati ya kura 690 zilizopigwa, Dk. Pallangyo aliibuka mshindi kwa kupata kura 470.

Ikumbukwe kuwa spika wa Bunge, Job Ndugai alitangaza jimbo la Arumeru mashariki kuwa wazi baada ya Nassari kushindwa kuhudhuria vikao vitatu vya Bunge mfululizo bila kutoa taarifa kinyume cha kanuni.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Aprili 7, 2019
LIVE: Rais Magufuli akizindua mradi wa ujenzi njia ya usafirishaji umeme

Comments

comments