Aliyewahi kuwa Mlimbwende wa taifa la Gambia mwaka 2014, Fatou Jallow amemtuhumu aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Yahya Jammeh kwa kumbaka na kumdhalilisha.

Jallow ametoa tuhuma hizo mbele ya Tume ya ukweli na maridhiao na kusema kuwa Jammeh ambaye mwanzo alijifanya kama mzazi, akimpa zawadi na ushauri, alimlazimisha amkatae mchumba wake ambaye walipanga kuoana.

“Nimejaribu kuficha hii stori na kuifuta kichwani kwangu lakini imeshindikana, sikupanga kuongea lakini nimeona ni wakati muafaka wa kusema, kile ambacho Rais jammeh alinifanyia ili Gambia na watu wengine wajue.

Yahya Jammeh aliikimbia nchi hiyo, Januari 2017 baada ya kushindwa katika Uchaguzi Mkuu na kukataa kutoka madarakani.

Mataifa ya Afrika Magharibi yaliingilia kati na Jammeh kutorokea Guinea Ya Ikweta ikiwa ni baada ya kukaa madarakani tangu mwaka 1994.

Serikali yawataka walemavu kusimama na kujipambania
EWURA yaja na mpango wa vituo vya mafuta vinavyotembea

Comments

comments