Kampuni ya Kilondo Investment imeanzisha mradi mkubwa wa umeme uliopo katika Kata ya Kilondo Wilayani Ludewa mkoani Njombe ili kuweza kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kupitia sera yake ya Tanzania ya Viwanda.

Hayo yamesemwa Wilayani Ludewa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Erick Mwambeleko ambapo amesema kuwa Kampuni hiyo inaundwa na vijana Wazawa wa Kata ya Kilondo Wilayani humo.

Amesema kuwa mradi wa umeme katika Kijiji cha Kilondo unategemea Chanzo Kikubwa cha Mto Kiwe ambao unatarajiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha Kilowati 100 hadi Megawati saba za umeme baada ya kukamilika kwake.

Aidha, uongozi wa kampuni hiyo umesema kuwa mradi huo ulianza rasmi Mwaka 2015 ambapo Lengo Iilikuwa ukamilike Mwaka 2017 lakini ulishindwa kukamilika kutokana na kukumbwa na ukata wa kifedha kwakuwa Pesa iliyotolewa na Serikali kupitia REA Kiasi cha shilingi Milioni 196 kwa awamu ya tatu imeisha na mradi huo kwasasa upo katika hatua za mwisho za ukamilishaji.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kilondo wamesema kuwa wataendelea kushirikiana na uongozi wa kampuni ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.

 

Wananchi wambana waziri kuchangia gharama za umeme
Video: Kwenye suala la fedha sinaga uvumilivu- JPM

Comments

comments