Rapper wa bongo Kherry Samir a.k.a Mr. Blue ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa ‘mbwa koko’ amedai kuwa sababu kubwa iliyompelekea kumtaja Ali kiba katika ngoma hiyo ni kutaka kujiweka mbali na wanawake wanaoshindwa kujistili.

Ameyasema hayo mara baada ya watu wengi kuuchukulia wimbo huo kama ‘diss track’ kwa wasanii ambao amewataja ndani ya ngoma hiyo.

Amesema kuwa alichofanya yeye ni majigambo na katika sanaa anayoifanya inamruhusu kufanya hivyo, kwa hiyo watu na mashabiki wasichukulie kama ‘diss’ kwa wasanii wengine.

“Nimetaja wimbo wa ‘seduce me’ kwa sababu kuna ‘line’ zinazungumzia jinsi ya wakina mama wanavyoshindwa kujistili, kwa hiyo mimi lazima nigeuke kama Alikiba uni-seduce kwa sababu hutoniweza kukaa na mimi ‘so seduce me like’ Alikiba. Mimi sija-disi mtu katika nyimbo yangu ila nimezungumzia changamoto za upande wangu wa ‘rap,”amesema Mr. Blue

Mourinho atamba kutwaa mataji EPL
Wajitolea kumkopesha Rais Trump ‘choo cha dhahabu’