Msanii wa maigizo ya uchekeshaji nchini, Brian Anaeli Mrikaria maarufu kama Mr Beneficial anayefanya kazi zake za uchekeshaji chini ya Timamu Media ambaye amepata umaarufu mkubwa kwa style ya kuchekesha kwa kuvaa uhusika wa Arusha.

Mr. Beneficial alipata nafasi ya kuzungumza juu ya sanaa yake katika media kubwa hapa duniani ya British Broadcasting Corporation (BBC), akisema kuwa yale maisha anayoigiza ni maisha ambayo amewahi kuyaishi.

”Yani kile unachokiona kwamba chalii niaje, ora nivipi kinichi kinachi yale ni maisha nimewahi kuyaishi katika muda nilioishi Arusha” amesema Mr. Beneficial.

Aidha Mr. Beneficial amesema sanaa ya uigizaji vichekesho ameanza kuifanya miaka mitatu iliyopita na kitu kikubwa kilichomsukuma kuingia katika sanaa hiyo ni kutokana na familia yake yote kuwa wachekeshaji.

Ameongezea kuwa hadhani kama anaweza kuacha uhusika huo kwani uhusika huo hauwezi kumzuia kufanya kitu kingine.

Hata hivyo kabla Mr Beneficial kuigiza kwa kuvaa uhusika wa Arusha alikuwa akivaa uhusika wa kimasai ambapo hakupata wafuasi wengi kama ambavyo amewapata hivi sasa.

 

 

 

Kansela wa Ujerumani ampigia simu JPM
Boomply yasaini mkataba na Warner Music

Comments

comments