Mshambuliaji wa Klabu ya TP Mazembe kutoka Congo DR, Tresor Mputu amesema kuwa anajua kwamba klabu ya Simba haifungiki ikiwa nyumbani lakini watajitahidi ili waweze kuondoka na ushindi.

Ameyasema hayo mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam na kupokelewa na mashabiki wa timu hiyo.

Klabu ya TP mazembe walitua katika Uwanja wa Ndege wa Songwe kabla ya kuwasili jijini Dar es salaam, ambapo imeelezwa kuwa walitua kwaajili ya kufanya matengenezo madogo.

Aidha, baada ya kutua Dar es salaam, wachezaji na viongozi walipokelewa na mashabiki wao waliojitokeza, ambao muda wote walikuwa wakiimba nyimbo za Kikongo na Kifaransa, shangwe lao liliongezeka zaidi baada ya kumuona mshambuliaji hatari wa klabu hiyo, Tresor Mputu ambaye ana mabao manne mpaka sasa katika Klabu Bingwa Ulaya.

Inaelezwa kuwa baada ya kutua, Mazembe waligomea basi kubwa lililoandaliwa na wenyeji klabu ya Simba, bali walitumia mabasi madogo mawili na basi waliloandaliwa lilitumiwa na mashabiki wao.

Wakati huo huo wenyeji wa mchezo, klabu ya Simba wameianza safari asubuhi ya leo kurejea Dar es salaam kutoka mjini Morogoro, kufuatia mchezo wao kuahirishwa Jumatano, April 3 baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha uwanja wa Jamhuri kujaa maji.

Mchezo huo wa Klabu Bingwa Afrika baina ya Simba na TP Mazembe utapigwa Jumamosi, April 6 katika Uwanja wa Taifa saa 10 jioni.

LIVE: Yanayojiri katika Ziara ya Rais Magufuli mkoani Mtwara
Ndugai atoa onyo kali kwa waandishi wa habari wa bungeni