Msanii wa muziki nyimbo za asili nchini ambaye ametamba sana na wimbo wake wa Sizonje, Mrisho Mpoto amefunguka juu ya msanii wa filamu maarufu kwa kuigiza sauti ya Hayati Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, Steve Nyerere mara baada ya kuponda tuzo za Filamu zilizoandaliwa na Azam.

Mpoto ameshangazwa na kitendo hiko kwani anaamini huo ni mwanzo mzuri wa kuinua tasnia ya filamu nchini kutokana na sanaa hiyo kufifia kwa siku za karibuni.

Amesema kuwa Steve ni moja kati ya watu waliojaribu kuua sanaa na anashangazwa kwa nini anakatisha tamaa watu wenye nia ya kurudisha tasnia ya filamu nchini.

Aidha amemuomba Steve apunguze gubu na waungane ili wawe kitu kimoja chenye heshima na cha kujivunia kwenye tasnia hiyo.

Mrisho amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa instagram, ambapo ameandika waraka mrefu kumkosoa Steve Nyerere,  amesema.

”Stive Nyerere Mbona huna Jema ndugu? Uzalendo ni Hali ya Mtu kujitoa kufa na kupona Kwa maslahi ya wengi yenye Tija Kwa Taifa, nikakusikia kwenye vyombo vya habari unasema Uzalendo ni project yako, tena ukaenda Mbali zaidi ukasema nimedandia project yako kwa mbele, nikahisi tofauti kidogo: Kwakua kilikua kipindi cha jua kali kidogo….Sasa hivi umeibuka na kuanza kuponda Tuzo za Sinema zetu ambazo ndiyo kwanza zinaanza ili kujaribu kurudisha Heshima ya filamu zetu ambazo wewe umechangia kufa kwake hauoni unakatisha tamaa watu wenye nia njema na Filamu? Ebu punguza gubu ndugu yangu angalau tuwe na kitu kimoja Chenye heshima cha kujivunia kwenye tasnia ya sanaa….ya uigizaji…zile Tuzo zilitolewa Kwa wenye Umiliki wa filamu na aliyewasilisha kwenye Mashindano na siyo anaeonekana sana kwenye Runinga…siyo lazima apewe unaemtaka wewe Stive. Najua kile kilikua kipindi cha jua, hiki cha mvua labda utanielewa kidogo…wadau na Mashabiki wa Bongo Movie msikatishwe tamaa”. amesema Mrisho.

Usiku wa pasaka, Azam kwa mara  ya kwanza iliandaa tuzo kwa wasanii wa filamu nchini waliofanya vizuri kupitia filamu zao, ambapo kupitia tuzo hizo wasanii mbalimbali walipokea tuzo akiwemo Wema Sepetu kupitia filamu yake ya Heaven Sent na Gabo kupitia filamu yake ya Safari ya Gwalu.

Kenya kuanzisha barabara za mwendo kasi
Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 12