Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina  ameridhia  maamuzi ya Kampuni ya Ranchi za NARCO kuvunja mkataba baina ya mwekezaji Agri Vision Global Ltd katika  ranchi ya Kagoma iliyopo mkoani Kagera na kuamuru aondoke mara moja baada ya mwekezaji huyo kushindwa kutekeleza mkataba katika kipindi cha miaka mitano.

Ameyasema hayo mara baada ya kutembelea ranchi hiyo kuangalia shughuli mbalimbali ambapo ametoa siku saba kwa mwekezaji huyo kuondoka katika eneo hilo.

“Ninakuagiza Mkuu wa Wilaya kuanzia sasa hakikisha unaimarisha ulinzi katika ranchi hii katika kipindi cha kukabidhi Ranchi baina ya Serikali na Mwekezaji ili kusitokee hujuma zozote,”amesema Mpina

Aidha Mpina ametoa siku saba  kwa uongozi wa NARCO kuhakikisha kuwa imefanya tathmini ya hasara zilizosababishwa na mwekezaji huyo ili taratibu za kisheria zichukuliwe dhidi yake, ikiwemo kuilipa Serikali shilingi bilioni kumi na tano kama gawio la miaka mitano iliyokaa ambalo amesema halijawahi kulipwa hata shilingi moja.

Hata hivyo, amewaonya wawekezaji kuacha tabia ya kuidanganya serikali kuwa wanauwezo wa kuwekeza katika vitalu ili wapewe lakini wanabadili matumizi baada ya kupewa.

 

Video: Man United yaichakaza CSKA Moscow
Kikwete afanya uteuzi