Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina, ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Singida kwa jitihada za kuweka mji huo kuwa safi tofauti na mikoa mingine ambayo amewahi kushiriki zoezi la usafi.

Ameyasema hayo mjini Singida mapema hii leo alipokuwa akishiriki siku ya usafi, Mpina amesema kuwa usafi wa mazingira  unapunguza magonjwa mbalimbali yatokanayo na uchafu kama ugonjwa wa kipindu pindu na hivyo taifa likiwa safi litaweza kuokoa nguvu kazi na kupunguza gharama ambazo zingetumika kutibu maradhi hayo.

“Ukiona Msichana mzuri barabarani ujue kagharamiwa ukiona kijana mtanashati vile vile ujue kagharamiwa Mkiona taifa zuri na safi ujue limegharamiwa na wananchi wake wamejipanga vizuri, hivyo wana singida Muendelee kujitahidi katika suala zima la usafi wa mazingira.” Alisema Mpina.

Zoezi la usafi wa Mazingira Mkoani Singida lilienda sambamba na zoezi la upandaji miti ambapo, Mpina, alishiriki  na wananchi katika zoezi la kupanda miti.

Makamba awataka vijana kutokuwa tegemezi
#HapoKale