Kiungo wa klabu ya Tottenham Moussa Sissoko hatoadhibiwa na chama cha soka nchini England (FA), kufuatia kosa alilolifanya wakati wa mchezo wa kwanza wa ligi kuu, uliowakutanisha na Newcastle  Utd mwishoni mwa juma lililopita.

Sissoko alimkanyaga kwa makusudi mshambuliaji wa pembeni wa Newcastle Utd Robert Kenedy Nunes Nascimento, aliyekua chini baada ya kuwania mpira wa kiungo huyo wa Ufaransa.

Tukio hilo halikuonwa na mwamuzi Martin Atkinson aliyechezesha mchezo huo, uliomalizika kwa Spurs kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja, zaidi ya picha za waandishi wa habari zilizosambaa katika mitandao ya kijamii.

Chama cha soka (FA) kimefuatilia picha hizo na kujiridhisha kuwa, Sissoko hakunanya tukio hilo kwa makusudi, na imeamua kumuacha aendelee na majukumu yake ya kuitumikia Spurs katika michezo ya ligi inayofuata.

Mabao ya Spurs katika mchezo huo yalifungwa na Jan Vertonghen na Dele Alli huku Joselu akifunga bao la kufutia machozi upande wa Newcastle Utd.

Video: Zitto avaana na Nape..., Chadema yaja na uamuzi mgumu
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 14, 2018