Manchester United watawakaribisha mahasimu wao Manchester City katika mchezo wa mzunguko wa nne wa michuano ya kombe la ligi nchini Uingereza.

Jose Mourinho na Pep Guardiola watatumia mchezo huo kuendeleza upinzani wao kwa mara ya pili msimu huu, na kama itakumbukwa vyema katika mchezo wa ligi ya nchini Uingereza Man City walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja mwanzoni mwa mwezi huu.

Wakati Mahasimu wa mji wa Manchester wakipangwa kukutana, huko jijini London kutakua na patashika nguo kuchanika kati ya West Ham dhidi ya Chelsea.

Norwich City walioitwanga Everton katika uwanja wa Goodison Park wamepangiwa kukutana na Leeds katika uwanja wa Elland Road, huku Preston ambao waliwasambaratisha Bournemouth watasafiri mpaka mjini Newcastle kupambana na Newcastle Utd.

Michezo ya mzunguuko wanne imepangwa kuchezwa Oktoba 24.

Ratiba ya mzunguuko wanne wa michuano ya kombe la ligi iliyopangwa na chama cha soka nchini Uingereza FA:

West Ham v Chelsea

Manchester United v Manchester City

Arsenal v Reading

Liverpool v Tottenham

Bristol City v Hull City

Leeds United v Norwich City

Newcastle United v Preston North End

Southampton v Sunderland

Ratiba hiyo ilipangwa saa chache baada ya michezo ya mzunguuko wa tatu jkuchezwa usiku wa kuamkia hii leo ambapo matokeo yalikua:

Fulham 1-2 Bristol City

Northampton 1-3 Man Utd

QPR 1-2 Sunderland

Southampton 2-0 Crystal Palace

Swansea 1-2 Man City

West Ham 1-0 Accrington

Stoke 1-2 Hull City

Tottenham 5-0 Gillingham

Diego Godin Amkalisha Messi, Kurejea Uwanjani Mwezi Ujao
Utafiti: 42% ya wanaume, wanawake Japan ni 'Bikira', Serikali yahaha...