Kocha wa Klabu ya Manchester United (Red Devil), Jose Mourinho amesema kuwa amefurahi kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kukinoa kikosi hicho kwani ana matumaini makubwa ya kutwaa mataji.

Mourinho alikuwa amebakiza mwaka mmoja kumaliza mkataba wake, hivyo ameaminiwa kuendelea kuifundisha timu hiyo hadi mwaka 2020.

“Najisikia mwenye thamani kupewa fursa ya kuendelea kuongoza kundi la vijana wenye ubora na uwezo mkubwa katika soka hivyo naamini tutafikia malengo ya timu,”amesema Mourinho

Hata hivyo, kocha huyo alijiunga na United mwaka 2016 kwa mkataba wa miaka mitatu ambapo ulikuwa unamalizika majira ya kiangazi mwakani, lakini sasa ameongeza mwaka mmoja hadi 2020 huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine mmoja.

Nikki wa Pili akanusha alichohoji Nassari
Mr. Blue akanusha 'kumdiss' Ali Kiba