Kocha wa Manchester United Jose Mourinho, amewataka mashabiki wa timu hiyo kujiandaa na burudani kwenye uwanja wa nyumbani wa Old Trafford, ambapo timu hiyo inatarajia kukwaana Chelsea.

Akizungumzia mchezo wa leo dhidi ya Chelsea, Mourinho amesema ana imani huo ni mchezo wa kwanza kati ya michezo mingine ambayo watacheza nyumbani ndani ya mwezi huu na Machi hivyo hana shaka kuwa watatumia vizuri uwanja wao.

“Nadhani wiki chache zijazo Old Trafford itashangaza, tuna mechi mbili kubwa za ligi, tutafanya vizuri dhidi ya Chelsea na Liverpool pamoja na mechi yetu ya ligi ya Mabingwa,”amesema Mourinho

Aidha, Baada ya mchezo wa leo dhidi ya Chelsea vijana wa Mourinho wataanza mwezi Machi na safari ya kwenda kucheza na Crystal Palace kabla ya kuwakaribisha Liverpool.

Hata hivyo, United itakuwa mwenyeji wa Sevilla kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa hatua 16 kabla ya kucheza robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Brighton. Man United kwasasa inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 56.

Viongozi Kenya watofautiana kauli kuhusu Utalii Tanzania
Marekani kuyawekea vikwazo mataifa yanayoshirikiana na Korea Kaskazini