Takribani watu 37 wameripotiwa kupoteza maisha katika hospitali ya Sejong nchini Korea Kusini baada ya moto kuzuka na kuteketeza jengo la wodi moja.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi nchini humo, moto huo ulianzia katika chumba cha dharura na baadae kuvamia jengo hilo. Mbali na vifo hivyo, watu 70 wanaripotiwa kuwa wamejeruhiwa vibaya kutokana na tukio hilo.

Imeelezwea kuwa wagonjwa 200 walikuwa ndani ya jengo hilo, na kwamba madaktari, wauguzi wengine pia walifariki kutokana na moto huo.

Tukio hilo la moto linatajwa kuwa tukio kubwa la vifo vitokanavyo na moto lililowahi kutokea nchini humo ndani ya kipindi cha muongo mmoja uliopita. Idadi ya vifo inahofiwa kuwa inaweza kuongezeka kutokana na hali ya baadhi ya waathirika kuwa mbaya.

Kwa mujibu wa ripoti ya The Daily JoongAng Ilbo, wataalam wa hospitali hiyo wamewapa kipaumbele zaidi watu wenye mahitaji maalum na wazee na kwamba baadhi ya wagonjwa waliokuwa wanatibiwa kwenye wodi hiyo walikuwa wagonjwa sana.

Mtoto wa Rais wa zamani atupwa jela kwa kutoa habari za uongo
Rais Kenyatta ‘awatuliza’ wanawake