Mwanamuziki maarufu nchini DR Congo aliyeimba wimbo wa ‘Papa Lolo’, Mose Se Sengo ‘Fan Fan’ amefariki dunia jijini Nairobi.

Mose Fan Fan amefariki akiwa na umri wa miaka 75 kutokana na mshtuko wa moyo.

Mwanamuziki huyo alikuwa mjini Nairobi kwa ajili ya kurekodi nyimbo mpya na wanamuziki wa Nairobi akiwemo Paddy Makani na Disco Longwa.

Katika taarifa ya gazeti la The standard nchini Kenya, mshindi wa tuzo ya kuchora wanasesere Paul Kelemba aka Mado amesema Mose alikuwa akicheza Gita na bendi ya Franco Ok Jazz mwaka 1972.

“Ninamtambua kuwa mchezaji Gita na mwandishi mzuri wa nyimbo barani Afrika . Amekuwa akizuru nairobi mara kwa mara tangu 2015 akishirikiana na na bendi ya Ketebul Music na tabu Osusa” amesema Mado.

”Tumeshangazwa na kifo chake na tunafanya mipango ya kumpeleka katika chumba kizuri cha kuhifadhi maiti huku tukiwasiliana na familia yake” wamenukuliwa mashabiki wa msanii huyo..

Mose amekuwa akiitembelea sana Kenya kila mwaka katika kipindi cha miaka mitatu iliopita kutoka London anakoishi.

Ndege ya Boeing 737 yatua mtoni ikiwa na watu 143
‘Dkt. Mwaka’ aeleza alivyofanya mazingaombwe hadi kuwa Tabibu