Mchungaji wa Kanisa la Mlango wa Ukombozi Gairo mkoani Morogoro, Joseph Gervas (28), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha tatu huku akitajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mama mzazi wa binti huyo.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchemba amethibitisha kukamatwa kwa mchungaji huyo ambaye aliwaaminisha wanawake na mabinti kuwa kwa kufanya nao mapenzi anawatoa mapepo.

Amesema binti aliyepewa mimba alikuwa na tatizo la macho ambalo lilisababisha kupata tatizo la kuanguka ndipo alipopelekwa na baba yake kwa mchungaji huyo kwaajili ya kuombewa.

Mchembe amesema mchungaji huyo alishauri familia kumuacha binti nyumbani kwake kwa siku kadhaa kwaajili ya maombi zaidi na ndipo alipoanza kumwingilia kimwili.

” Huko kwenye maombi kulikuwa na mabinti wengine wawili ambao walikuwa wanafanyiwa hivi, lakini huyu mmoja ndiyo alikubali kusema wazi, alitaka kusema kabla lakini mama yake alikuwa akimzuia” Amesema DC Mchemba.

Na kuongeza ” Mwanafunzi huyo aliamua kumweleza baba yake na baba alivyokuwa mkali kwa mama yake na binti ndipo mama wa binti ilithibitisha kuwa na mahusiano na mchingaji huyo”

Amesema mchungaji huyo alikuwa akienda nyumbani kwa familia hiyo mara kwa mara wakati baba wa familia hayupo na alikuwa akipikiwa vyakula kama nyama na chapati.

Gazeti la nipashe limemnukuu DC Mchemba kuwa “Ndugu wa mume walistushwa na mazoea hayo na walipofuatilia walibaini jambo na kumweleza ndugu yao (baba)”.

” Kwa nyakati tofauti alikuwa anaenda kufanya maombi ya chumvi nyumbani kwa wahusika, pia alikuwa anazunguka nyumba za watu hapo kijijini hasa wanawake” amebainisha Mkuu huyo wa Wilaya.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa anadaiwa kuwa aliwaaminisha wanawake hao anatoa mapepo kwa kushiriki nao tendo la ndoa wakati mwingine kuweka dawa kwenye sehemu zake za siri na kuwaingilia.

Katika mkutano wa hadhara wanawake wengi walisimama na kuanza kueleza vitendo vya udhalilishaji waliofanyiwa na mchingaji huyo kila walipokwenda kanisani kwake.

Hadi sasa mtuhumiwa huyo yupo siku ya tatu korokoroni kwaajili ya usalama wake kutokana na wananchi wa eneo hilo kuwa na hasira kiasi cha kutaka kumdhuru.

Mtuhumiwa mkuu mauaji ya Kimbari akana mashtaka "sijaua Watusi wowote"
Masau Bwire ahofia Ligi Kuu kuchezwa Dar es salaam