Msanii wa filamu nchini Yvone Cherly maarufu kama Monalisa amepata fursa ya kushiriki tuzo kubwa zinazotolewa nchini Ghana zijulikanazo kama The African Prestigious Awrds akiwania kama msanii bora wa kike tasnia ya filamu Afrika akiiwakilisha Tanzania.

Kipengele hiko  kinachogombaniwa na wasanii wengi wa kike kutoka nchi mbalimbali za Afrika zikiwemo, Nigeria, Tunisia, Morocco, Kenya, South  Africa, Algeria, Zimbabwe na  Ethiopia.

Ambapo kwa upande wa kiume kutoka Tanzania tuzo hiyo itashindanishwa na Vincent Kigosi maarufu kama Ray, huku wapinzani wake wakiwa ni wasanii kutoka mataifa mengine ya Afrika.

Aidha Monalisa kupitia ukurasa wake wa instagram ametoa shukrani zake za dhati kwa uongozi kwa kumchagua kugombania tuzo hiyo, hivyo amewaomba watanzania kumpigia kura ili aweze kurudisha tuzo hiyo nyumbani.

Msanii wa maigizo ya Soga na mwanamitindo anayekuja juu na brand yake ya viatu  IdrissSultan for Men, Idriss Sultan ametumia ukurasa wake wa instagram kuhamisisha mashabiki na wazalendo kumpigia kura mwanadada huyo Monalisa.

Hata hivyo kwa upande wa maigizo ya vichekesho Idriss amepigwa chini kuwania kinyang’anyiro hiko baadala yake  mzee majuto anawania kipengele hiko akishindanishwa na wasanii wengine kutoka nchi za Afrika.

Tuzo hizi hutolewa kwa kushindanisha vipengele mbalimbali nchini Afrika vyenye ubora vikiwemo, blogu, Tv Chaneli, banki, Dj, makampuni makubwa, wasanii wa filamu, na maigizo ya vichekesho pia  kwa kuzingatia Vigezo ambapo lengo kubwa la tuzo hizi ni kusapoti sekta mbalimbali zilizofanikiwa katika shughuli wanayofanya na kuleta maendeleo Afrika.

Kuwa mzalendo kwa kuwapigia kura watanzania waliopendekezwa kuwania tuzo hizo kwa kubonyeza  link hapa chini.

 

 

Polisi wawili wafariki Jijini Mbeya
Afungua kesi mahakamani akitaka ukeketaji uhalalishwe