Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya ⁦Simba SC Mohamed Dewji ⁦ amerejea kwenye nafasi ya Uenyekiti baada ya jana kutangaza kujiengua kufuatia kipigo cha 1-0 kwenye fainali ya MapinduziCup2020 dhidi ya ⁦Mtibwa.

MO Dewji jana alifikia maamuzi mazito ya kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti na kubakia kama muwekezaji wa Simba.

MO alifikia hatua hiyo kutokana na timu hiyo kutofanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakitolewa na UD Songo ya Msumbiji hatua ya awali, sare ya 2-2 dhidi ya Yanga inayoonekana kupitia kipindi kigumu kiuchumi na kupoteza fainali ya leo ya Mapinduzi Cup 1-0 dhidi ya Mtibwa.

Leo Mo ameamua kuachana na hasira za maumivu ya kufungwa na kuamua kurudi kwenye nafasi yake ambayo awali alitangaza kujiuzulu nafasi yake na kusema kuwa kilichotokea kwenye akaunti zake jana  kilikuwa ni bahati mbaya na yeye ni simba damu bado wapo pamoja.

Image may contain: text that says 'Mohammed Dewji MO @moodewji What happened to my accounts yesterday was unfortunate. Tuko pamoja. We're going back to the league strong. Tunajipanga kwaajili ya ligi. Nawapongeza Mtibwa kwa kuchukuwa kombe. Mimi ni SIMBA damu damu. Nitabaki kuwa SIMBA! #NguvuMoja'

“Kilichotokea kwenye akaunti zangu jana kilikuwa ni bahati mbaya, tuko pamoja, tunarudi kwenye ligi tukiwa na nguvu , tunajipanga kwa ajili ya ligi, nawapongeza Mtibwa kwa kuchukua kombe, mimi ni Simba damudamu, nitabaki kuwa Simba” – MO DEWJI

Mvua zatajwa kutosaidia joto kushuka nchini
Kigwangalla ahoji bilioni 4 alizotumia Mo kwa wanasimba