Naibu waziri wa Kilimo, Omary Mgumba amewataka wananchi kutambua kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya rais Dkt. John Pombe Magufuli imefanya vizuri katika kutekeleza majukumu yake na Ilani yake ya uchaguzi wa mwaka 2015 tofauti na propaganda za baadhi ya watu wanavyodai.

Ameyasema hayo katika vikao vya wajumbe wa CCM, maeneo ya Kinole. Tegetero na Kibungo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Mkoani Morogoro.

Akizungumza na wajumbe hao kwa nyakati tofauti, Mgumba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini Mashariki, amesema kuwa serikali imefanya mambo mazuri katika kuwahudumia wananchi wake katika Jimbo hilo la Morogoro Kusini Mashariki.

Aidha, ameongeza kuwa baadhi ya miradi hiyo katika kipindi cha Miaka mitatu ya serikali ya awamu ya tano katika jimbo hilo ni pamoja kuunganisha mitandao ya barabara, kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa vituo vya afya, umaliziaji wa maboma na ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja mabweni ya wanafunzi.

Katika hatua nyingine, Mgumba amewataka wananachama wa chama cha Mapinduzi CCM kueleza mazuri yanayofanywa na serikali kwani wasipofanya hivyo baadhi ya watu wenye chuki na chama hicho wanaweza kueneza propaganda chafu.

Pia ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wanachama hao kuchagua viongozi wenye uchungu na CCM pamoja na wenye kujali maslahi ya wananchi watakaoenda kuwahudumia vizuri.

 

Magogo ya kukatia Nyama buchani yapigwa marufuku
Mbunge Neema Mgaya akabidhi vifaa vya michezo mkoani Njombe