Mmiliki wa Lori lililotelekezwa katika machinjio ya ng’ombe Jijini Dar es salaam eneo la Tegeta likiwa na mizoga 12 ya ng’ombe anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi.

Taarifa hiyo imetolewa rasmi na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhanga Mpina leo Mei 16, 2018  jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda CCM aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya wahusika wa tukio hilo.

Amesema mmiliki wa machinjio ilikokutwa mizoga hiyo ametoroka na Serikali inaendelea kumtafuta ili afikishwe katika vyombo vya sheria.

Kwa mujibu wa Waziri Mpina lori hilo lilikuwa na ng’ombe 54 wakiwamo wazima 42 na mizoga 12 na ng’ombe 4 wakiwa wamechunwa ngozi.

Tukio la kuonekana kwa lori hilo lenye ng’ombe vibudu 12 lililotokea usiku wa kuamkia jumapili Mei 13, mwaka huu Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es salaam jirani na machinjio.

BOT Yaziunganisha benki ya Twiga na Benki ya TPB
Kenya yapata mwarobaini wa uhalifu wa mtandaoni