Leo katika mkutano wa 15 kikao cha 6 cha bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga alihoji juu ya suala la kutoa motisha kwa wakuu wa Wilaya na Mkoa wanaofanya vizuri.

Akiuliza swali hilo amewataja baadhi ya wakuu wa wilaya na mkoa ambao wanastahili kupata motisha kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataja Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Salum Hapi  na Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti kwa ubunifu mkubwa wa kukabiliana na kutatua matatizo ya wananchi.

Akijibu swali hilo Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo amesema kuwa tayari suala hilo lipo katika ajenda za vikao vinavyoendelea kwani ni kweli anatambua juhudi zinazofanywa na baadhi ya wakuu wa mikoa na wakuu wilaya kwani kwa kiasi kikubwa matatizo mengi ya wananchi yamepungua.

”Nikili wazi kweli kuna wakuu wa mikoa hivi sasa wanaofanya kazi vizuri sana, ajenda ya kuwapa ‘apriciation’ kwa baadhi ya wakuu wa mikoa tumeshaanza kuifanya katika vikao vyetu, na juzi baadhi ya wakuu wa mikoa tumewapa vyeti” amesema Jafo.

Aidha Jafo ameongezea kuwa kufuatia mradi ulianzishwa hivi karibuni ambao ulihusisha ujenzi wa viwanda 100 kwa kila mkoa ambapo mradi huo ulitekelezeka na kupitiliza malengo ambapo matarajio yalikuwa kufanyika kwa ujenzi wa viwanda 2600 na hadi kufikia sasa kuna ujenzi wa viwanda 4877.

”Tulianzisha programa ya ujenzi wa viwanda kwa kila mkoa matarajio yetu ni kupata viwanda 100 kwa kila mkoa, matarajio yetu ni kupata viwanda 2600 lakini tumepata viwanda 4877 ni outstanding perfomnce na kazi hii imesimamaiwa na wakuu wa mikoa.

Hivyo amewashukuru Wakuu wa Wilaya kwa kusimamia vyema mradi huo.

LIVE: Rais Magufuli katika uzinduzi wa kituo cha afya Madaba - Ruvuma
Video: Maajabu 5 michuano ya AFCON 2019 | Tanzania imetajwa kwenye hili

Comments

comments