Mkurugenzi wa zamani wa Katani Limited, Salum Shamte amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya mifupa (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Agosti 2019 akiwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Salum Shamte alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza jipya la Biashara la SADC.

Taarifa ya Msemaji wa MOI Patrick Mvungi inaeleza kuwa Kiongozi huyo aliwasili hospitalini hapo Machi 23 mwaka huu akitokea Gereza la Maweni Tanga ambapo alikuwa ameshikiliwa kwa tuhuma za uhujumu uchumi zinazojumuisha kosa la utakatishaji fedha.

Kutoka kwa familia, Mariam Shamte amesema kuwa mume wake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo, na kwamba amefanyiwa upasuaji mara kwa mara.

Mnamo siku ya Alhamisi Oktoba 31, 2019, Salum Shamte pamoja na wenzake walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga na kukabiliwa na mshataka matatu.

Mashtaka hayo ni ya Uhujumu Uchumi, utakatishaji fedha na kusababisha hasara ya Tsh. Bilioni 1.14 kwa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS).

Somalia yatuma madaktari 20 kuongeza nguvu Italia
LIVE: Hali ya Corona Duniani