Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa kuna miradi mikubwa takribani miatano (500) inaendelea nchi nzima ambayo inapeleka maji vijijini na mijini.

Ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa na mkutano wa mapitio ya sekta ya maji, Jijini Dodoma huku kauli mbiu ya maadhimisho hayo ikisema ‘’ hakuna atakaye achwa nyuma kuongezeka kasi ya upatikanaji wa huduma ya maji na usafi wa mazingira kwa wote katika dunia inayobadilika kitabia nchi’’

Aidha, Mbarawa ameongeza kuwa wanaendelea na malengo, kwamba itakapofika mwaka 2020 kwa maeneo ya miji mikuu ya mikoa lazima wafikie asilimia 95 .

Katika hatua nyingine amesema kwenye sekta ya maji ni kweli kulikuwa na changamoto  kubwa za usimamiaji wa miradi lakini wametengeneza sheria mpya ya usafi na huduma ya mazingira ya mwaka 2019.

Kwa upande wake Mhandisi, Dorisia Mulashani ambaye ni Mkurugenzi  wa uratibu wa programu ya sekta ya maji amesema kuwa katika wiki ya maji wamefanya shughuli za aina tatu ambayo ni kwaajili ya maadhimisho ya wiki ya maji kwanza walianza siku ya tarehe 18-19  mwezi machi ambapo kulikuwa na kongamano la kisayansi kwaajili ya wataalamu wa sekta ya maji.

Hata hivyo, kila mwaka  wadau kutoka serikalini, wafadhili na asasi mbalimbali hukutana pamoja kupitia ufanisi wa sekta ya maji  na usafi wa mazingira, ambapo mtandao wa asasi zinazofanya kazi katika sekta ya maji na usafi wa mazingira nchini TAWASANET hufanya uangalizi wa maendeleo sekta ya maji kupitia uandaaji wa ripoti ya usawa.

 

Ghana yaongoza kutengeneza majeneza yenye mvuto, yatazame hapa
Taifa Stars kuweka historia

Comments

comments