Meneja wa mabingwa wa soka nchini England Man City Pep Guardiola ameanza kukutana na vikwazo kuelekea kwenye kampeni za kutetea taji lake msimu ujao, baada ya kiungo aliyemsajili Douglas Luiz Soares de Paulo kushindwa kupata kibali cha kufanyia kazi.

Guardiola alikua na matumaini ya kuanza kumtumia kiungo huyo kwenye mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Arsenal utakaochezwa katika uwanja wa Emirates kaskazini mwa jijini London, lakini hatoweza kufanya hivyo kutokana na mamlaka za England kushindwa kujiridhisha katika suala la kumpatia kibali cha kufanyia kazi nchini humo.

Douglas alikua napewa nafasi kubwa ya kuziba pengo la kiungo mwenzake kutoka Brazil Fernandinho, lakini kutokana na changamoto zilizomkabili, hatokua na budi ya kupelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Girona ya Hispania ama sehemu nyingine.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, alicheza kwa mkopo akiwa na Gerona msimu uliopita, baada ya kusajiliwa na Man City mwaka 2017 akitokea Vasco da Gama,na kukutana na vikwazo vya kukosa kibali kwa mara ya kwanza.

Kwa mantiki hiyo Guardiola atalazimika kusaka mbinu mbadala za kukipanga kikosi chake kuelekea mchezo wao wa kwanza dhidi ya Arsenal, na tayari fununu zinaeleza huenda akamtumika John Stones kama kiungo mkabaji akisaidiana na Fabian Delph.

Fernandinho, ambaye alipaswa kucheza katika nafasi hiyo, kwa sasa hayupo kwenye kiwango chake kilichozoeleka na meneja huyo kutoka nchini Hispania amedhamiria kumpa muda ili kufanikisha mpango wa kuwa FIT kabla ya kumrudisha katika kikosi cha kwanza.

Habari Picha: Rais Dkt. Magufuli akutana na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza
Jamie Vardy yupo King Power Stadium hadi 2022