Michuano ya Tennis inayoendelea jijini London nchini Uingereza ya Wimbledon Open, usiku wa kuamkia leo iliingia dosari baada ya viashirio vya moto kusikika kwenye jumba la uwanja wa Centre Court.

Kiashirio hicho kilionekana kuwapa hofu maafisa wa uwanja huo ambapo walihaha huku wakiwasihi mashabiki kuwa wastahamilivu na kutoka uwanjani hapo kwa utaratibu.

Balaa hilo lilijitokeza mara baada ya mchezo uliomkutanisha mwanadada kutoka nchini Marekani, Serena Williams dhidi ya mshiriki kutoka nchini Hungary Tímea Babos ambaye alikubali kufungwa kwa seti mbili kwa sifuri ambazo ni 6–4 na 6–1.

Hata hivyo ,waandishi wa habari walitakiwa kubaki uwanjani hapo kwa utaratibu wa kuchukua taarifa na picha za tukio hilo, lakini baadae ilibainika kuwa hakukuwa na madhara yoyote.

Kikosi cha zima moto kilifika eneo la tukio kwa lengo la kutoa huduma na dakika chache kuwa hakukuwa na hatari ya moto bali kulikuwa na hitilafu ndogo za mitambo ya uwanja huo.

Lakini pamoja na kubainika kwa dosari za miundombinu ya uwanja wa Centre Court, bado taarifa rasmi za kuendelea kwa michezo ya hii leo ama kuahirishwa hazijathibitishwa na vyombo husika.

Blatter: Nitakapoingia Peponi Ndipo Mtaamini Sikutafuna Rushwa
Msikiti Wachangia Fedha Kukarabati Kanisa Lililoharibiwa Na Muislam