Kwa mwaka wa sita sasa Michael Jackson ameendelea kuikalia namba moja ya orodha ya watu maarufu waliopoteza maisha ambao wanaingiza pesa nyingi zaidi.

Kwa mwaka huu 2018 amefanikiwa kuingiza kiasi cha Dola million 400.

Mkali wa Pop mrehemu, Micheal Jackson aliyefariki dunia mwaka 2009 ameingiza kiasi hicho cha zaidi ya billioni 917 za kitanzania tangu October 2017 hadi 2018.

Kiasi kikubwa cha pesa zake kimetokana na mauzo ya asilimia 50 za haki za kazi zake kutoka kampuni ya EMI Music Publishingi kwenda Sony/TV ambapo asilimia 10 ilienda kwa familia yake.

Mauzo mengine ya ziada kutoka kampuni yake ya  Mijac Catalog (MMC) pia haki za Television kwa kuruhusu kituo cha CBS kuonesha kipindi cha Micheal Jackson Halloween kwa miaka miwili mfululizo .

Aidha, katika orodha hiyo Mrehemu XXTentacion ameingia kwenye nafasi ya kumi na moja akiingiza kiasi cha dola milioni 11 huku Elvis Presley akishika nafasi ya pili akiingiza dola million 40 huku aliyekuwa mwanamuziki mkongwe wa rege duniani Bob Marley akishika nafasi ya tano  akiingiza dola milioni 23.

RC Makonda aunga mkono mradi wa TACIP
Video: Foby aeleza alivyomlilia mpenzi studio, ‘Niokoe’

Comments

comments