Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Urambo mkoani Tabora imewahukumu watu watatu kutumikia kifungo cha miaka miwili jela kwa kila mmoja kwa kosa la kuuza dawa za binadamu ambazo muda wake wa matumizi umekwisha.

waliokutwa na hatia katika kosa hilo ni Mbyeti Magese, Eliud James na Peter Maneno wote wakazi wa kijiji cha Mwamnange wilayani Urambo.

Baada ya kuridhishwa na upande wa mashahidi katika kesi hiyo Hakimu Mfawidhi, Hassan Momba alitamka hukumu ya miaka miwili jela kwa kila mtuhumiwa wa kosa hilo au kulipa faini ya sh. 550,000/= kwa kuuza dawa zilizokwisha muda wake na kutokuwa na kibali.

Washtakiwa hao walikamatwa januari 21, mwaka huu baada ya kufanyika msako katika kata na vijiji vya wilaya hiyo, katika mduka ya madawa kutafuta watu wanaokiuka sheria za kuuza dawa za binadamu.

 

Waathirika wa VVU Songea waanzisha mradi wa ufugaji kuku
Video: Ridhiwani Kikwete akabidhi mradi wa maji safi na salama

Comments

comments