Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) aliyeibua mijadala mitandaoni baada ya kudai kwamba rushwa ya ngono imekithiri chuoni hapo ameitwa kwenye kamati ya maadili ya chuo hicho.

Dkt. Vicensia Shule alikuwa ameandika kwenye Twitter kwamba alitaka sana kuufikisha ujumbe wake kwa Rais Dkt. John Magufuli lakini alizuiliwa na walinzi wake.

Aidha, Rais Dkt. Magufuli alienda chuoni hapo kufungua maktaba mpya, kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

Maktaba hiyo kubwa Afrika Mashariki na Kati ilijengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 93.6 ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya China na ndiyo maktaba kubwa kuliko maktaba zote ambazo China imezijenga barani Afrika.

“Nimepigiwa simu kuitwa kwenye Kamati ya Maadili siku ya Ijumaa 30 Nov mchana. Nasubiri mwaliko rasmi kwa maandishi, kwa manusura wa udhalilishaji huu wa kingono, tunakaribia kufika, tutashinda, tutapata ushindi mkubwa,”ameandika Dkt. Shule

Hata hivyo, tamko lake lilizua mjadala mtandaoni, baadhi wakikubaliana naye na wengine kumwambia angetumia tu ujasiri na kutimiza azma yake.

Video: Hoja saba kuwatoa Mbowe, Matiko leo? Rushwa ya ngono UDSM yachukua sura mpya
Serikali kulipa bilioni 4 kila siku kwa wakulima wa Korosho