Rushwa ya ngono imekithiri katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambapo mhadhiri mmoja wa chuo hicho amemuomba rais Dkt. Magufuli kuingilia kati.

Mhadhiri huyo ameyasema hayo katika mtandao wake wa kijamii baada ya rais Dkt. Magufuli kuzindua maktaba ya kisasa ya chuo hicho.

Dkt. Vicencia Shule ambaye ni mhadhiri chuoni hapo amemuomba rais Magufuli kuingilia kati suala hilo kwakuwa alizuiliwa kuonyesha bango lake chuoni hapo.

“Baba rais Dkt. Magufuli, umeingia chuoni hapa kuzindua maktaba hii mpya na ya kisasa, Rushwa ya ngono imekithiri sana hapa UDSM, nilitamani nikupokee kwa kukuonyesha bango langu, lakini ulinzi wako umenifanya ninyamaze, nasubiri kutoka kwako maana wateule wako naamini ni waadilifu watakwambia ukweli,”ameandika Dkt. Shule

Aidha, kauli hiyo imeibua mijadala mkubwa katika mitandao ya kijamii ambapo wachangiaji wengi wamesema kuwa si chuo kikuu cha Dar es salaam tu bali rais Dkt. Magufuli aingilie vyuo vikuu vyote kwani malalamiko yamekithiri kote.

Hata hivyo, baadhi ya wachangiaji wameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM), kimekuwa kama Dangulo la kujiuza kwa watoto wa kike.

Kaka wa rais akamatwa na dawa za kulevya
Papa Francis ateua mrithi wa muda wa Askofu Chengula

Comments

comments