Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia kwa Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed imethibitisha kisa cha tatu cha mgonjwa wa Corona na kufanya idadi ya walioambukizwa kufikia 14 kwa Tanzania.

Mgonjwa huyo ni mwanamke raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 57. Mwanamke huyo alirejea Zanzibar akitokea Uingereza na shirika la ndege la Qatar.

Hadi kufika sasa ni mgonjwa mmoja wa covid 19 ambaye ametangazwa kupona ni mmoja ambaye ndiye alikuwa wakwanza kugundulika akiwa mkoani Arusha.

 

Uganda: Waliothibitika kuwa na virusi vya Corona wafikia 23
Corona Kenya: Mapadri na waumini wakamatwa kwa kushiriki Ibaada

Comments

comments