Raia wa Kenya aliyeaga dunia siku ya Alhamisi nyakati za mchana katika chumba cha wagonjwa mahututi hospitali ya Agha Khan jini nairobi ambako alikua amelazwa alikuwa anaugonjwa wa kisukari.

Raia huyo mwenye umri wa miaka 66, alikuwa amewasili nchini Kenya tarehe 13 mwezi Machi kutoka Afrika Kusini kupitia Swaziland.

Katika taarifa iliotiwa saini na waziri wa Afya Mutahi Kagwe, serikali ilisema kwamba ilipokea kwa huzuni habari za kifo cha Mkenya huyo ambaye alikuwa amekutwa na virusi hivyo baada ya kupimwa.]

Katika mkutano na wanahabari afisa mkuu katika wizara ya afya Mercy Mwangangi alisema kwamba visa vyote vya hivi karibuni ni vya Wakenya waliokaribiana na watu walioripotiwa kuwa na ugonjwa huo hapo awali.

Rais Uhuru Kenyatta alitangaza hatua kadhaa ambazo alisema zitasaidia serikali yake kukabili janga la corona ikiwa ni pamoja na amri ya kutotoka nje kuanzia Ijumaa Machi 27 kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.

Ummy Mwalimu: ''Makonda amemkosea Mbowe''
Aliyeua mfanyakazi Arusha apandishwa kizimbani, aongezewa shtaka la Mirungi

Comments

comments