Kampeni za Uchaguzi Mkuu nchini Uganda zimeendelea kuvutia hoja mbalimbali na ahadi kutoka kwa wagombea ambazo baadhi zimekumbwa na vipingamizi vya wazi.

Mgombea urais wa Uganda anaeshindana na Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi wa mwaka huu, Amama Mbabazi ameahidi kuurudisha mwili wa Dikteta Idi Amin Dada aliyekuwa rais wa nchi hiyo kabla ya kuondolewa kwa nguvu na majeshi ya Tanzania mwaka 1979 kupitia vita ya Kagera.

Id Amin alikimbilia nchini Libya na baadae kuelekea nchini Saudi Arabia ambapo aliishi uhamishoni hadi alipofariki mwaka 2003 na kuzikwa huko.

Mbabazi ameahidi kuurudisha mwili wa Iddi Amini na kujenga jumba la makumbusho kulizunguka kaburi lake atakapozikwa upya.

Msemaji wa Mbabazi, Bi. Josephine Mayanja-Nkangi amesema kuwa moja kati ya vipaumbele vya chama chao ni kuhakikisha inawaleta pamoja Waganda kusamehe na kusahau yaliyopita, na kwamba suala la Iddi Amin ni mojawapo.

Hata hivyo, Viongozi wa dini ya Kiislam nchini humo wamepinga ahadi ya mgombea huyo wakieleza kuwa inakinzana na imani yao.

Msemaji wa Baraza Kuu la Waislamu Uganda Hajj Nsereko Mutumba ameambia BBC kwamba haamini kama Mbabazi alikuwa na nia ya dhati alitoa ahadi hiyo, kwakuwa dini ya Kiislamu haikubali mwili wa mtu kufukuliwa na kuzikwa tena.

Picha: Hawa ndio wake 10 wa marais wa Afrika, wanaotajwa kuwa wazuri zaidi
Ligi Daraja La Pili Kuendelea Wikiendi