Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai, 2018 umepungua hadi kufikia asilimia 3.3 ikilinganishwa na asilimia 3.4  mwezi Juni, 2018.

Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo alipokuwa akitoa taarifa ya mfumuko wa bei kwa mwezi Julai mwaka huu.

Amesema kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2018.

“Kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 kumechangiwa hasa na kupungua kwa mfumuko wa bei wa baadhi ya bidhaa za vyakula, ambapo bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei kati ya Julai, 2017 na Julai 2018 ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 9.5, Mtama kwa asilimia 17.8, Unga wa Mihogo kwa asilimia 14.1, Matunda jamii ya Machungwa kwa asilimia 22.2, Maharagwe kwa asilimia 5.8 na Mihogo mibichi kwa asilimia 12.5,” amesema Kwesigabo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki umeongezeka akianza kuitaja Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 umeongezeka hadi asilimia 3.1 kutoka asilimia 2.2 kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018. Kwa upande wa Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 umeongezeka hadi asilimia 4.35 kutoka asilimia kutoka asilimia 4.28 kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2018.

 

Video: Hali ilivyokuwa baada ya JPM na Kikwete kukutana kwenye msiba wa 'King Majuto'
Video: Vijana fanyeni kazi acheni kulalamika - Majaliwa