Kocha wa Simba, Pierre Lechantre ambaye ni raia wa Ufaransa amepewa jukumu zito la kuhakikisha anaifikisha mbali timu hiyo kwa kufanya vyema katika michuano ya kimataifa.

klabu ya Simba haijatwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara  kwa miaka kadhaa, lakini mwaka jana ilipatra nafasi hiyo baada ya kushinda Kombe la FA kwa kuifunga Mbao FC katika fainali.

Hivyo, inatarajiwa kushiriki katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambayo inatarajiwa kuanza mwezi wa pili mwaka huu.

Uongozi wa timu hiyo unatarajia kuwa na kikao kizito mara siku yoyote  kwa ajili ya maandalizi katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

Simba itacheza mchezo wake wa kwanza wa kimataifa katika michuano hiyo ya kimataifa dhidi ya Gendarmerie Nationale ya Djibout mnamo Februari 11, baada ya kutoshiriki kwa miaka minne mfululizo.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa mipango hiyo ilipangwa kabla ya mchezo wao dhidi ya Majimaji, uliochezwa Jumapili iliyopita ambapo Simba ilishinda mabao 4-0.

Nia ya kikao hicho ni kuhakikisha Simba inafanya vizuri kimataifa kama ilivyo kawaida yao ilipokuwa ikishiriki miaka ya nyuma. Ikumbukwe pia Simba ilitolewa katika Kombe la FA, hatua ambayo ilisababisha hata kumfukuza kocha Joseph Omog.

Magazeti ya Tanzania leo Januari 31, 2018
Tebas atamani kumrudisha Neymar Hispania