Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema kuwa mchango mkubwa unaotolewa na wakina mama katika kujiletea maendeleo ni mkubwa zaidi hivyo amewataka akina baba kuwaunga mkono ili kuharakisha shughuli za maendeleo katika jamii.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa vikundi vya wanawake iliyofanyika katika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es salaam, amesema kuwa wakina mama ndio msingi mkubwa ndani ya familia na Taifa kutokana na mchango wao.

Amesema kuwa licha ya changamoto wanazokutana nazo lakini wamekuwa si watu wa kukata tamaa hivyo amesisitiza akina baba kuwaunga mkono ili waweze kufikia ndoto zao za kujiletea maendeleo.

 

Aidha, ameongeza kuwa katika shughuli za maendeleo hakuna mambo ya vyama na kwamba viongozi waliopo kwenye nafasi zao, wanatakiwa kuwatumikia wananchi wote ili kuhakikisha kwamba wanatimiza ahadi zao za kuleta maendeleopata maendeleo katika jamii.

“ Kwenye suala la maendeleo hakuna mambo ya vyama, kila mmoja anahitaji maendeleo, mambo ya vyama hivi sasa tunayaweke kando,  ili kupata muda wa kufanya kazi moja tu, ya kuwatumikia wananchi ambao mmetuchagua,”amesema Mwita.

 

Video: Hasira tano za Lowassa kwa Serikali, CCM, Waziri amtaka Kitwanga ahame chama
Magazeti ya Tanzania leo Mei 14, 2017