Meya wa  manispaa ya Iringa nchini Tanzania , Alex Kimbe ameondolewa madarakani  na wajumbe wa baraza maalum la madiwani katika halmashauri hiyo leo machi 28, 2020.

Kimbe anatoka chama cha democrasia na maendeleo (Chadema), ameng’olewa madarakani mara baada ya kura kupigwa ambapo mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni naibu Meya wa manispaa ya Iringa Joseph Ryata amesema wajumbe waliohudhuria kikao ni 26 na kura 14 zimeridhia kumuondoa Meya huyo.

”Ndugu zangu wajumbe kura zilizopigwa ni 26 kura zilizoharibika ni 12 kura halali ni 14 na kura za ndio ni 14 na hapana ni sifuri, hivyo baraza la leo limepiga kura kihalali na taratibu zote zimezingatiwa”amesema Ryta.

”kuanzia leo machi 28, 2020 Alex Kimbe hatakuwa meya hadi taratibu zitakavyofuata na baada ya kusema hayo naomba mkurugenzi uhairishe kikao” amesema

Hata hvyo kabla ya kupiga kura hizo mkurugenzi wa manispaa hiyo Hamid Njovu alitoa utaratibu wa kupiga kura wa kumuondoa Meya huyo.

Corona Kenya: Mapadri na waumini wakamatwa kwa kushiriki Ibaada
Membe: ''Tusipuuzie Corona tutaumwa na wengine tutakufa''